Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe akipokea nyaraka mbalimbali za utendaji kazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kikao kazi hicho na menejimenti ya Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es salaam
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa kikao kazi baina ya menejimenti ya Ofisi hiyo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe (hayupo pichani) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe (hayupo pichani) kilichofanyika jijini Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na uongozi na menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na viongozi wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB) walipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Kumbukeni Kondo akimsilikiza mwananchi mwenye mahitaji maalumu ndugu Semeni Lutaja alipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho vya Dkt. John Samuel Malecela, Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Baraka Luvanda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho vya Dkt. John Samuel Malecela, Jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dkt. Juma Homera wakati akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Arusha.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) alipowasili kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere kutembelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhusu Hassan akipokea maelezo kutoka kwa Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi kuhusu namna Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inavyotekeleza majukumu yake wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) uliofanyika Jijini Arusha.