Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

Serikali Yashinda Shauri la Usuluhishi Katika Baraza la Kimataifa la Biashara (ICC)

25 October, 2024 Pakua

Tarehe 06 Machi, 2024, Baraza la Kimataifa la Biashara (International Chamber of Commerce-ICC) limetoa uamuzi wake na kuipa Serikali ushindi katika Shauri la Usuluhishi Na. 2682/AZO baina ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (Petroleum Bulk Procurement Agency-PBPA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Kampuni ya Alchemist Energy Trading DMCC kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu.