Majukumu ya Vitengo
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ina vitengo saba (7) kama ifuatavyo;
Kitengo hiki kinahusika na usimamizi wa rasilimali fedha, kitengo hiki kinahusika na majukumu yafuatayo; kuingiza malipo kwenye mtandao (Data entry); kutunza nyaraka mbalimbali za uhasibu zikiwemo fedha (Cashoffice); kushughulikia masurufu ya safari na masufuru maalum (Safari and Special imprest); na ukaguzi wa nyaraka mbalimbali kabla ya kufanya malipo (Pre-Audit).
Kitengo hiki kinahusika na kutoa ushauri kwa Afisa Masuuli kuhusu matumizi sahihi ya rasilimali za ofisi.
KITENGO CHA MANUNUZI NA UGAVI
Kitengo hiki kinahusika na kutoa ushauri wa kitaalamu, kufanya manunuzi mbalimbali, na utunzaji wa vifaa (Store) katika OWMS kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 pamoja na Kanuni za Mwaka 2013 na mabadiliko yake ya Mwaka 2016.
KITENGO CHA TEHAMA
Kitengo hiki kinahusika na usimamizi na matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika OWMS.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
Kitengo hiki kinahusika na kutoa ushauri kuhusu masuala ya habari na mawasiliano katika OWMS.
KITENGO CHA MASIJALA YA SHERIA
Kitengo hiki kinahusika na upokeaji, usajili, usambazaji na uhifadhi wa majalada na nyaraka mbalimbali za mashauri ya madai na usuluhishi ya ndani na nje ya nchi.
KITENGO CHA HUDUMA ZA MAKTABA NA UTAFITI
Kitengo hiki kinahusika na kutoa ushauri, kusimamia maktaba na kuhakikisha rasilimali zilizomo zinatunzwa na kutumika kwa mujibu wa taratibu.