Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akizungumza na Rais wa Taasisi ya Usuluhishi Tanzania Bi. Madeline Kimei (hayupo pichani) alipotembelea Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende (kushoto) akimkabidhi Jarida la Wakili Mkuu Rais wa Taasisi ya Usuluhishi Tanzania, Bi Madeline Kimei alipofika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujitambulisha.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi Sarah Mwaipopo (aliyesimama kushoto) na Rais wa Taaisisi ya Usuluhishi Tanzania, Bi. Madeline Kimei baada ya kumaliza kikao.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Sarah Mwaipopo akizungumza na Mawakili Wafawidhi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali waliopo mkoani Tanga wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao cha kujadili utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo.
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete, Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimuapisha Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Dkt. Boniphace Nalija Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Boniphace Luhende Wakili Mkuu wa Serikali akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Sara Mwaipopo, na wajumbe wa Menejimenti wa Ofisi hiyo baada ya viongozi hao kuwasili Ofisini hapo muda mfupi baada ya kuapishwa.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akizungumza na wajumbe wa Baraza la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Slyvester Mwakitalu, akizungumza na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria kutoka Wizara, Taasisi za Umma, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini wakati wa kikao kazi chao kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji. Dkt. Eliezer Feleshi akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria wa Wizara mbalimbali, Taasisi za Umma, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini kilichofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akizungumza na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria kutoka Wizara , Taasisi, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini wakati wa kikao kazi kilichofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali wa Mikoa mbalimbali kutoka Ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria nchini.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT na TBA na watumishi wa OWMS wakati wa makabidhiano ya eneo kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende akikata utepe kwa ajili ya makabidhiano ya nyaraka za ujenzi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inayotarajiwa kujengwa katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Watumishi walioshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali mara baada ya kufungua kikao cha Pili cha Baraza la Wafanyakazi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Nalija Luhende, akipata elimu ya afya na upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza, VVU/UKIMWI na utoaji chanjo ya UVIKO 19 kutoka kwa Mtaalamu wa afya kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam.
Wanawake kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kwenda uwanja wa Uhuru kuungana na wanawake wenzao nchini kwa lengo la kushiriki Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.
Balozi Ombeni Sefue akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka OWMS, walioshiriki mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu ipasavyo kwa kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama ya Tanzania baada ya kuzindua Juzuu za Sheria na kampeni ya kuhamasisha watumishi wa Mahakama kuchanja chanjo ya kujikinga dhidi ya UVIKO
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Nalija Luhende alipomtembelea ofisi kwake hivi karibuni.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Nalija Luhende, akisisitiza jambo wakati wakizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Idara ya Usuluhishi George Mandepo akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali Erigh Rumisha (kulia) na Zakaria Kakwaya (kushoto) wakijadili moja ya Shauri wanaloliendesha.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu James Kibamba akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Idara hiyo wakati wakifuatilia namna Mfumo wa taarifa za kiutumishi unavyofanya kazi.
30th Nov 2022
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ameweka jiwe la msingi kwenye jengo jumuishi la taasisi za kisheria linalojengwa eneo la Bus... Soma zaidi
Soma zaidi