Watumishi wa umma ni taswira au sura ya Serikali hivyo tunatakiwa tuangalie na kuzingatia namna tunavyofanya kazi na tunapotekeleza majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa niaba ya Serikali. Kila mmoja ana wajibu kwa kutunza taswira ya Serikali tunayoitumikia chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Soma zaidiWakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza kwa njia ya mtandao na waajiriwa wapya wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa mafunzo elekezi yaliyofanyika mkoa wa Pwani.
Soma zaidiWakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi ametoa wito kwa taasisi zote za kisheria na wadau wa haki nchini kutumia mifumo ya kidijitali kupata takwimu sahihi zitakazowawezesha kufuatilia migogoro yote waliyoisikiliza ili kuhakikisha inamalizika kwa mafanikio.
Soma zaidiWakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi amefungua kikao kazi cha wadau wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OWMS) cha kupitia na kutoa maoni kuhusu Kanuni za Urejeshaji wa Gharama za Uendeshaji Mashauri ya Serikali kilichofanyika mkoa wa Pwani.
Soma zaidiWananchi wametakiwa kuendelea kupata elimu kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu licha la Mahakama kuruhusu waleta maombi katika shauri linalopinga mamlaka ya Waziri wa TAMISEMI kutunga kanuni za kuratibu, kusimamia nakuendesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini kuruhusiwa kufungua shauri la msingi kwa kuwa mchakato mzima wa uchaguzi haujasimamishwa.
Soma zaidi