WAKILI MKUU WA SERIKALI ASHIRIKI UAPISHO WA MAWAKILI WAPYA
WAKILI MKUU WA SERIKALI ASHIRIKI UAPISHO WA MAWAKILI WAPYA
Imewekwa: 12 December, 2024
Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi ameshiriki sherehe za uapisho wa Mawakili wapya 524, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam mapema leo tarehe 12 Disemba 2024.
Aidha, Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Mhe. Sylivester Mwakitalu na Viongozi wengine wa Serikali.
Mgeni Rasmi katika sherehe hizo alikuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.