Habari

Imewekwa: May, 27 2022

​Rais Samia: Nitaboresha Maslahi Ya Wafanyakazi Nchini

News Images

Rais Samia: Nitaboresha Maslahi Ya Wafanyakazi Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuboresha maslahi ya watumishi nchini kwa lengo la kuinua hali zao za kiuchumi ili waweze kumdu gharama za Maisha.

Mheshimiwa Rais ametoa ahadi hiyoleo wakati akizungumza na Watumishi mbalimbali waliojitikeza katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Katika kuhakikisha ahadi hiyo inatekelezeka Rais Samia ameagiza kufanyika kwa majadliano yatakayokuwa na lengo la kuimarisha maslahi ya wafanyakazi kati ya Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) na Serikali ili kujua kiwango sitahiki cha maslahi kinachohitajika kuongezwa.

“Serikali imeshaunda Bodi za kima cha chini cha mshahara kwa sekta zote yaan sekta binafsi na ile ya Umma na tayari zimeshaanza kufanya kazi tathimini ya mishahara iliyopo sasa ili kujua ni kiwango gani kinatakiwa kuongezwa”. Alisema Rais Samia.

Aidha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Maafisa Rasilimali watu kwa kushirikiana na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kushughulikia mapema haki na stahiki za watumishi wanaotarajia kustaafu ndani ya miezi sita ili mtumishi anapofika muda wa kusitaafu mafao yake yawe tayari yametoka hatua itakayosaidia kuondoa usufumbu miongoni mwa wasitaafu nchini.

Akizungumzia watumishi waliofanya kazi kwa muda mrefu na kisha kufukuzwa kazi kwa sababu ya vyeti feki, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kushughulikia stahiki zao zinazotokana na Makato ya Mishahara yao ili waweze kulipwa kwa kuwa serikali inatambua mchango wao walioutoa kipindi walichotumikia Taifa.

Kuhusu namna Serikali ilivyoendelea kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa umma kote nchini Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali imeendelea kustawisha maslahi ya wafanyakazi tangu mwaka 2021 ikiwepo kupunguza makato ya kodi, kuongeza umri wa wategemezi kutoka miaka 18 mpaka 21, kupandisha vyeo vya watumishi, kubadilisha kada, kulipa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi pamoja na kutoa ajira mpya zilizosaidia kujaza nafasi mbalimbali zilizokuwa wazi na hivyo kuongeza ufanisi katika maeneo mbalimbali nchini.

Nayo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeshiriki Maadhimisho hayo ikiongozwa na Mwenyekiti wa TUGHE, tawi la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mtani Songorwa ambapo waeungana na Watumishi kutoka sehemu mbalimbali nchini kushiriki Maadhimisho hayo kwa maandamano yaliyopita mbele ya Mgeni Rasmi wakiwa na mabango yenye jumbe zinazolenga kuonyesha mshikamano baina ya watumishi, Vyama vya Wafanyakazi na Serikali yakisindikizwa na kauli mbiu isemayo “Mishahara na Maslahi Bora kwa wafanyakazi ndio Kilio chetu: Kazi iendelee”.