Timu ya Mpira wa Miguu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (Wakili Mkuu Sports Club), imefanikiwa kuiduwaza timu ya mpira wa miguu ya Wakala wa Serikali Mahala pa Kazi (OSHA) baada ya kibuka na ushindi wa bao 1-0 Katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mabatini jijini Mwanza.
Soma zaidiTimu ya wanawake wa Ofisi ya Wakili Mkuu Wa Serikali, imefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupata alama moja kati ya alama mbili zinazotakiwa katika mzunguko wa kwanza wa mchezo wa kuvuta kamba wakati wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini mwanza.
Soma zaidiWakili Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Ally Possi akiwa kwenye kikao na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kupokea kompyuta mpakato 30 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, ndugu Mohammed Khamis Abdulla kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Ofisi hiyo kwenye hafla iliyofanyika leo Wizarani, Mtumba, Dodoma.
Soma zaidiWakili Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Ally Possi (kulia) akifurahia kupokea kompyuta mpakato 30 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ndugu Mohammed Khamis Abdulla kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo Wizarani, Mtumba, Dodoma.
Soma zaidiWakili Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Ally Possi (kushoto) akipokea kompyuta mpakato 30 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ndugu Mohammed Khamis Abdulla kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo Wizarani, Mtumba, Dodoma.
Soma zaidi